Amos 2:6-8

Hukumu Juu Ya Israeli

6 aHili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Israeli,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Wanawauza wenye haki kwa fedha,
na maskini kwa jozi ya viatu.
7 bWanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,
kama vile juu ya mavumbi ya nchi,
na kukataa haki kwa walioonewa.
Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,
kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.
8 cWatu hulala kando ya kila madhabahu
juu ya nguo zilizowekwa rehani.
Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo
ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.
Copyright information for SwhNEN